Msanii wa filamu na tamthilia Mwijaku, ameeleza sababu ya yeye kutupiana maneno katika mitandao ya kijamii na msanii mwenzake Irene Uwoya.


Mwijaku amesimulia hayo kupitia EATV & EA Radio Digital baada wawili hao kujibizana kwa maneno katika mtandao kijamii wa Instagram hivi karibuni.

“Si unajua sisi wanaume bwana, kabla sijaoa nilikuwa napenda kutongoza,sasa kile kitendo kilinifanya kujichomeka mahali, kwa hiyo kwa ile tabia alitaka kuweka wazi ili kuniharibia ndoa yangu kwa sababu ya kutongoza na kumtongoza na yeye”, amesema Mwijaku.

Aidha Mwijaku ameeleza kuwa Irene Uwoya hawezi kumuharibia kwa sababu kutongoza kwa wanaume ni jambo la kawaida na amekataa kusema kama alikubaliwa au alikataliwa baada ya kumtongoza Irene.

Irene Uwoya aliwahi kumuonya Mwijaku kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram kwa akisema kuwa asimfuatilie maisha yake kwa sababu hapendi maneno na ana maovu yake mengi anayoyajua.