Moja kati ya story kutoka ‘Lebo’ ya WCB ambazo zinasambaa mtaani kwa kasi ni story ya Harmonize kujiengua katika lebo hiyo na kuanzisha Lebo yake.  Kwa nyakati tofauti Harmonize amekuwa akikanusha tetesi hizo na kuwataka waandishi wanaouliza sana kuhusu suala hilo waache kufocus kwenye ‘mambo negative’ na badala yake waangalie mambo yanayojenga zaidi.

Baada ya tetesi hizo kusambaa, huku wahusika wakikanusha kwa zaidi ya mara moja, kuna mabadiliko ameyafanya Harmonize katika ukurasa wake wa Instagram ambayo ni moja kati ya ishara ambazo zinaashiria kuwa Harmonize huenda akaachana na Lebo hiyo iliyo chini ya Msanii Diamond Platnumz.


Ukurasa wa Instagram wa Harmonize ukiwa na Hauna Maelezo ya ‘Signed Under WCB Label’
Kabla ya hizi tetesi kusambaa, Harmonize pamoja na wasanii wengine wote wa WCB walikuwa wakitumia ‘Description’ inayosomeka ‘ Signed Under WCB Lebel ‘, Kitu ambacho Harmonize amekiondoa kwenye Bio ya Ukurasa wake wa Instagram na Kuacha Hashtag ya #WCB4LIFE

Tazama Kurasa za wasanii wote walio chini ya Lebo ya WCB, tofautisha na Kurasa ya Harmonize