Tyson ateketeza mamilioni ya pesa kwenye bangi
Bondia maarufu Duniani Mike Tyson mwenye miaka 53 kwa sasa, amefunguka suala lake la kahamia katika biashara ya bangi pamoja na matumizi ya bidhaa hizo.


Licha kustaafu mchezo wa ngumi mwaka 2005, Bondia huyo amekuwa ni mtangazaji wa kipindi cha “Hotboxin with Mike Tyson” pamoja na mshirika mwenziye aitwaye Britton ambapo amesema, “huwa tunatumia kiasi cha Milioni 91 za Tanzania katika utumiaji na uvutaji wa bidhaa hizi za bangi, pia tunatumia tani 10 kwa mwezi kwenye bangi tu, ni bangi nyingi sana kila sekunde lazima tuwe nayo”.

Aidha Mike Tyson ameeleza kuwa ana shauku kubwa ya kuingia katika biashara hiyo ya bangi na tayari ameshanunua ekari 40 kwa ajili ya kuzalisha bidhaa hizo ambazo zitaitwa Tyson Ranch na itapatikana Jijini California.

Pia ameendelea kwa kusema wameshawekeza kiasi cha bilioni 1 katika kukuza, kuzalisha, kusambaza kutangaza biashara hiyo.

Watu wengine maarufu ambao wameingia katika biashara hiyo ya bangi niJay Z, Snoop Dogg, Wiz Khalif