NAHODHA wa Yanga, Mkongo Papy Kabamba amejipanga kushinda dhidi ya Township Rollers na akasisitiza wanahitaji kupata mabao ya mapema zaidi kwenye mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.Yanga Jumamosi itakuwa Gaborone kurudiana na Township Rollers ukiwa ni mchezo wa marudiano wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare 1-1.Kwenye mchezo huo Yanga inahitaji ushindi au sare ya kuanzia mabao 2-2 ili kusonga hatua ya kwanza ya michuano hiyo. Akiwa Gaborone, Tshishimbi alisema wamejipanga kushinda na hakuna kitu kingine zaidi
ya ushindi sababu ndiyo utawapeleka hatua inayofuata.


“Tupo hapa Gaborone langu ni ushindi tu na kocha amesisitiza kuwa tunatakiwa kupambana ili kupata mabao ya mapema zaidi ili tuwe kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele.“Sababu mchezo huu na Rollers ni kama ilivyo michezo mingine na kocha ametueleza nini ya kufanya kwa kuhakikisha haturuhusu bao kutoka kwa wapinzani wetu kwa kuwa kwetu kinachohitajika ni ushindi tu na sio kitu kingine,”alisema Tshishimbi.Yanga inashiriki michuano hiyo sawa na Simba ambayo itakuwa na kibarua siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa dhidi ya UD Songo