Saa kadhaa baada ya kutokea kwa ajali ya boti iliyohusisha wafanyakazi 11 wa Benki ya NMB Korogwe, iliyopata dhoruba na kupinduka majini ambapo awali walifanikiwa kuokolewa watu 10, Jeshi la polisi limethibitisha kufariki Dunia kwa mtu mmoja.


Kwa mujibu wa Meneja wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) mkoani Tanga, Christopher Mlelwa amesema aliyefariki anajulikana kama Patrick Kiungulia, ambaye mwili wake ulipatikana baada ya kuendeshwa kwa zoezi la kuutafuta mwili huo, na jeshi la maji kwa zaidi ya saa 16.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe amewataka wanaotumia bahari kuwa makini katika kipindi hiki, ambacho bahari imekuwa ikichafuka mara kwa mara.