Amepigwa bao! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mrembo, Tanasha Donna ambaye ni mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kuonekana amefanyiwa makubwa na mpenzi wake huyo na kumwacha mbali mzazi mwenza na staa huyo, Hamisa Mobeto ambaye ndio alitangulia.  Tanasha ambaye ni raia wa Kenya anatarajia kupata mtoto na Diamond ambapo licha ya kwamba bado hajazaa lakini ameshampiga bao mara tatu Mobeto ambaye alitangulia kuzaa na Diamond.

“Hivi mnajua mpaka sasa Mobeto ameshapigwa bao na Tanasha maana si kwa kufuru hizo ambazo Mondi ameshamfanyia na leo kwenye Baby Shower tunatarajia makubwa kama alivyoahidi,” alisema shabiki wa Tanasha aitwaye Jamila.

Bao la kwanza ambalo Tanasha amempiga Mobeto kwa Diamond ni lile la kufanyiwa bonge la sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa ‘bethidei’ iliyofanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ambapo waalikwa waliinjoi vilivyo kutokana na sherehe hiyo ilivyokuwa. Hakuna kumbukumbu yeyote ya Mobeto kufanyiwa pati ya kuzaliwa na Mondi.

APEWA GARI LA KIFAHARI

Bao la pili ni kuzawadiwa gari la kifahari aina ya Toyota Prado TX ambalo thamani yake ni zaidi ya shilingi milioni mia moja za kitanzania.

BABY SHOWER LEO

Kama hiyo haitoshi, bao lingine ni sherehe kubwa ya baby shower inayotarajiwa kufanyika leo ambayo Diamond amesema itakuwa ni ya kifahari na haijawahi kutokea. Wakati Tanasha akifanyiwa hayo kwa upande wa Mobeto ambaye alitangulia kuzaa na Diamond amewahi kuambulia gari aina ya Toyoya RAV4 toleo jipya na kodi ya nyumba anayoishi kwa sasa.


“Mobeto hakufanyiwa makubwa, sijui ni kwa sababu alikuwa mchepuko kwani hata hiyo nyumba aliwekwa baada ya kumpeleka Mondi mahakamani, lakini angalia Tanasha amempiga bao 3 kwa muda mfupi tu, acha tuone picha linavyoendelea,” alisema Jamila. Gazeti la Amani linamtakia kheri Tanasha kwenye sherehe yake ya Baby Shower ambayo inatarajiwa kufanyika leo kwenye Hoteli ya Best Western Coral Beach Hotel jijini Dar.