Syria imeushutumu msafara huo kama kitendo cha uchokozi na imesema kwamba inaelekea katika eneo linalodhibitiwa na waasi la Khan Sheikhoun
Shambulio la angani la serikali ya Syria uliolenga msafara wa kijeshi wa Uturuki uliokuwa ukielekea katika eneo linalotawaliwa na waasi kaskazini mwa Syria limesababisha vifo vya raia watatu, Uturuki imedai.

Watu wengine 12 walijeruhiwa katika shambulio hilo katika mkoa wa Idlib siku ya Jumatatu kulingana na wizara ya ulinzi ya Uturuki.

Idlib ambayo ni mojawapo ya maeneo machache yasiodhibitiwa na serikali, ilitarajiwa kulindwa na kuwa eneo huru linalotenganisha majeshi pinzani lililoafikiwa na Uturuki inayowaunga mkono waasi mwaka uliopita.

Athari za uonevu wa shule za malazi
Ukatili wa mashambulio ya tindikali
Maneno matatu yanayoweza kuokoa maisha yako
Lakini mashambulizi ya serikali yamekuwa yakiongezeka tangu mwezi Aprili.

Mamia ya raia wameuawa kutokana na hilo na kuna hofu kwamba wengi watafariki iwapo hali itaendelea kuwa mbaya.

''Hii ndio hatari inayotukabili kwa sasa'', alisema Jan Egeland kutoka baraza la wakimbizi la Norway akizungumza na BBC.

Kwa miaka kadhaa sasa tumeonya kuhusu hatari inayoikabilia Idlib , ambapo hakuna mahala pa kutorokea kwa raia milioni 3.

Kuna wapiganaji wabaya mjini humo. Lakini shambulio la jumla katika eneo hilo pamoja na lile lililomkabala la kaskazini mwa Hama litamaanisha kwamba watoto milioni moja wataathiriwa na vita hivyo na hicho ndicho tunakiona kikifanyika

Kwa nini Uturuki inatuma msafara wa kijeshi nchini Syria?
Uturuki inayounga mkono baadhi ya waasi na sio wote ina majeshi yake Idlib kama mojawapo ya makubaliano na Urusi mwaka uliopita.

Kulingana na Naji Mustafa , msemaji wa waasi wa National Liberation Front msafara huo ulikuwa ukielekea katika mojawapo ya vituo vyake vya uchunguzi na walinzi wakati shambulio hilo lilipotokea,

Mwandishi wa AFP ambaye aliuona msafara huo anasema ulishirikisha magari 50 ya kijeshi , matano kati yao yakiwa vifaru.

Lakini Syria imesema kuwasili kwa msafara huo katika eneo hilo ni kitendo cha uchokozi . Imesema kuwa silaha hizo hazitasitisha harakati za wanajeshi wa Syria kukabili kile ilichokitaja kuwa magaidi.

Kulingana na Shirika la haki za kibinadamu la Syrian Observatory for Human Rights (SOHR), lililo na makao yake nchini Uingereza , ndege ya kijeshi ya Urusi ilitekeleza mashambulio karibu na msafara huo tarehe 19 Agosti.

Uturuki imesema kuwa shambulio hilo linakiuka makubaliano ya mwaka uliopita huku kisa hicho kikizua hofu kuhusu makubiiano ya moja kwa moja kati ya mataifa hayo mawili.

Kwa nini shambulio hilo lifanyike?

Baada ya miaka minane ya vita , serikali ya Syria inajaribu kuyakomboa maeneo yanayodhibitiwa na waasi.

Vikosi vya serikali vinavyoungwa mkono na Urusi , viliripotiwa kuingia eneo la kaskazini magharibi la Khan Sheikhoun siku ya Jumapili.

Eneo la Khan Sheikhoun ambalo lilishambuliwa na gesi aina ya sarin mwaka 2017 lipo katika barabara kuu inayounganisha Damascus na Aleppo na ni eneo muhimu la kimkakati kusini mwa mkoa huo.

Iwapo litakombolewa , itamaanisha kwamba utawala wa Syria umefanikiwa kulizunguka eneo linalodhibitiwa na waasi upande wa kusini ambalo linashirikisha kituo cha uchunguzi cha Uturuki katika mji wa Morek.