MSANII wa filamu Bongo, Diana Kimari ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani amefunguka kuwa hana mpango wa kurudi Bongo hivyo watu watamsikia tu.Akizungumza na Gazeti la Ijumaa kwa njia ya simu, Diana alisema hakuna kitu kizuri kama kujiepusha na walimwengu ambao kila kukicha wanakuweka midomoni mwao hivyo huko aliko ametuliza akili kwani hakuna anayemjua wala kumfuatilia.“Kwa kweli najisikia amani sana na Bongo watanisikia tu maana nikirudi watakuwa wameshanisahau kama nilikuwepo mtu kama mimi maana niliyachoka maneno yao,” alisema Diana.

Stori: Imelda Mtema