Tumepiga stori na msanii Lulu Diva "Diva Divana" amefunguka suala la zima la kutotumia kinga, kutongozwa na wanaume wengi kwa siku pamoja na kumkana Rich Mavoko.

Lulu Diva ambaye ni msanii wa BongoFleva na filamu, amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital ambapo amesema,

"Mimi na Mavoko hatujawahi kuwa na mahusiano. Kuhusiana na suala la kinga hapana, mimi na mpenzi wangu tayari tumeshapima na nina mpenzi mmoja tu".

Aidha Lulu Diva amesema kwa siku huwa anapokea DM meseji 100, 200, hadi 300 kutoka Wanaume kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, wakimtaka kimapenzi ila kwa bahati nzuri au mbaya huwa hasomagi na hafatilii hizo meseji.

Lulu Diva ambaye ni ndugu wa mchekeshaji Idris Sultan, kwasasa anatajwa kuwa na mahusiano na msanii na mbunge wa jimbo la starehe nchini Kenya Jaguar.