'Sitaki kuharibika ukubwani' - Mwana FA
Msanii nguli wa Hip Hop nchini, Mwana FA amesema wasanii wengi wamekuwa wakijibu kashfa mbalimbali zinazowakumba katika kutafuta kiki.


Mwana FA amesema hayo kwenye Friday Night Live “FNL” ya EATV, baada ya kuulizwa kuhusu kukwepa kwake kujibu kashfa anazohusishwa.

“Nikiwa na kashfa nitaijibu, bahati nzuri Mungu amenisaidia sinaga kashfa, kuna kashfa zinazokuja tu na ambazo zinatengenezwa, miaka yote hii nimekuwa nimefanya ninachofanya bila kashfa na ukianza sasa hivi unakuwa unaharibikia ukubwani kashfa haziendani na mimi”, amesema Mwana FA.

Aidha msanii huyo ambaye ni mjumbe wa bodi ya Baraza la sanaa la Taifa, amezungumzia suala la BASATA la kuonekana katika matukio ya kinidhamu kama kuwafungia wasanii kuliko matukio mengine.

“BASATA lina vitu vingi sana kama kusimamia sera ya sanaa ya Taifa, sheria zinazoongoza na yeye ni mjumbe tu wala sina mamlaka ya kuwaamrisha viongozi, kuhusu kutoa adhabu au kufungia nyimbo za wasanii” amesema Mwana FA