Simiyu : Mashine ya Ultra Sound na Printer zaibwa
Jumla ya watuhumiwa wanne wamekamatwa kutokana na shutma za wizi wa mashine ya 'Utrasound', iliyoibwa katika hospitali ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.


Akizungumza na EATV & Radio Digital, leo Agosti 15, 2019, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, William Mkonda, amesema jeshi la polisi linaendelea na upelelezi na mara baada ya upelelezi kukamilika watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

''Taarifa zipo kweli na zinafanyiwa kazi na ofisi ya RTO, uchunguzi ukikamilikia tutawafikisha washtakiwa mahakamani na tunawashikilia wanne'', amesema RPC Mkonda.

Mashine hiyo inadaiwa kuibiwa pamoja na kifaa chake cha kudurufu picha (printer), ambayo ilitolewa na wadau wa maendeleo UNFPA, maalumu kwa matumizi ya wodi mpya ya akina mama wajawazito na iliibiwa ikiwa kwenye wodi hiyo.