Shilole Siwezi Kufa na Unafiki
MSANII wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amesema watu wengi wanakwama kwa sababu hawapendi kusema ukweli badala yake wanakumbatia unafiki, jambo ambalo yeye hawezi kufa nalo.  Katika mahojiano na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Shilole alisema kama wanamuziki wangesema ukweli, basi kila mmoja angepata nafasi ya kufanya shoo kwenye matamasha ya wanamuziki wakubwa, lakini kwa kuwa wanaogopa ni ngumu kuendelea.

“Nilisema wazi kabisa kuwa WCB wanabagua wasanii kwenye tamasha lao la Wasafi, kama itawachukiza basi, lakini mimi siwezi kufa na unafiki,” alisema Sh ilole ambaye ni mama nt’ilie wa kishua.