Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally ametangaza kuwa sikukuu ya Idd El-Adh'haa itakuwa siku ya Jumatatu, Agosti 12, 2019.


Swala ya Eid kitaifa itaswaliwa katika viwanja vya Masjid Kibadeni, eneo la Chanika Zogowali, Ilala Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Baraza la Eid hapohapo katika viwanja vya Masjid Kibadeni mara baada ya swala kumalizika. Sheikh Mkuu anawatakia Waislamu na Watanzania wote sikukuu njema na anawaomba kusheherekea kwa amani.