Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajab, amesema waumini wa Dini ya Kiislamu nchini hawana budi kuliombea Taifa, katika kipindi hiki kigumu, ambacho kinachopitia hasa kuhusiana na matukio ya ajali yanayotokea hivi sasa.


Sheikh Mustafa ametoa kauli hiyo wakati wa ibada ya Idi iliyofanyika mkoani humo, ambapo amesema wakati waislamu wakisherehekea sikukuu ya Idi hawana budi kuwaombea marehemu na majeruhi wa ajali ya Morogoro.

Aidha Sheikh huyo amewataka Waislamu wote kujiandaa na kifo kwa kumcha mwenyezi Mungu mara kwa mara maana hawajui wakatyi wala saa ambao Mungu atawachukua.

Aidha sheikh Mustafa amewataka waislamu kuepukana na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe, ndani ya Misikiti.