Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imenunua magari kumi na mbili kwa ajili ya huduma za dharura nchini.

Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa wizara hiyo Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipofanya ukaguzi kwenye ofisi za Toyota jijini Dar es Salaam.

Dkt. Ndugulile amesema magari hayo yameletwa muda muafa ikiwa zimesalia siku chache kuanza mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo magari hayo pamoja na mabasi mawili ya uokozi yatatumika kutoa huduma za kiafya kwenye mkutano huo na baada ya hapo yatagaiwa kwenye maeneo yaliyoanishwa kwa uokoaji wa majeruhi wa ajali.