VIDEO queen na msanii wa filamu za Kibongo, Sasha Kassim ameibuka na kueleza jinsi anavyopitia kwenye wakati mgumu kukwepa vishawishi vya wanaume wanaomsaka ili kumlipizia kisasi kufuatia kauli yake.  Miezi kadhaa iliyopita, Sasha alikaririwa akisema kuwa hawezi kutoka na wanaume wa Kibongo kwa sababu ni wachafu.

Akichonga na Shusha Pumzi, Sasha alisema kuwa kauli yake hiyo imemfanya ajishtukie na kila mwanaume anayemuomba kuingia naye kwenye mapenzi inabidi amchunguze kwani wengi wana nia ya kumpata ili wampige picha za ngono na kuziachia mitandaoni.

“Unajua ni ukweli niliitoa ile kauli kwa sababu mbali na hivyo pia ninaye mpenzi wangu ambaye yupo nje ya nchi, lakini nimekuwa nikipandiwa dau na kushawishiwa kupelekwa Dubai ila nimewashtukia,” alisema Sasha