Kufuatia Sintofahamu Iliyokuwa Imetanda Kuhusu Hatma ya Msanii Harmonize Katika Lebo Yake ya WCB Wasafi, Mmoja Kati ya Mameneja wa Lebo hiyo Sallam sk Ameweka Wazi Ukweli Kuhusu Kinachoendelea!.

Sallam Amesema
 "Harmonize Ndani ya Moyo Wake Hayuko WCB, Lakini Kimakaratasi Yuko WCB, Harmonize Ametuma Barua ya Maombi ya Kuvunja Mkataba wake WCB na Yuko Ridhaa Kupitia Vipengele Vyote vya Sheria ili kuweza Kuvunja Mkataba Wake." .

Sallam Ameendelea Kwa Kusema Kuwa Wamependezwa na Maamuzi hayo ya Harmonize Kutokana na Kwamba yeye Mwenyewe Ameridhia na Kuamua Kufuata Sheria.