MUIGIZAJI wa Bongo Muvi, Husna Idd ‘Sajenti’ amesema kuwa kamwe kitu ambacho hawezi kukifanya ni ‘kumlamba miguu’ mwanaume ambaye amezaa naye kutoa matumizi ya mtoto wake wakati anajua amezaa.  Akizungumza na Amani, Sajenti alisema kuwa amekuwa ni mwanamke mwenye ‘roho ya chuma’ kwa sababu amekuwa akipambana na malezi ya watoto wake mwenyewe kwa vile baba zao wamejisahau kama wana majukumu ya kulea watoto wao.

“Kitu ambacho siwezi kukifanya mimi ni kumlamba mwanaume ambaye anajua wazi kuwa amezaa sehemu hivyo siwezi kujisumbua kwa sababu mwisho wa siku watoto ni wa mama,” alisema Sajenti

Sajenti alizaa mtoto wake wa kwanza na mwanamuziki wa The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ na mtoto wake mwingine amezaa na muigizaji wa Bongo Muvi, Gabo Zigamba. Walipotafutwa wazazi wenza hao na Amani simu zao ziliita bila kupokelewa hadi tunakwenda mitamboni