WIKI chache baada ya Meneja wa WCB, Sallam kusema kuwa staa wa Bongo Fleva, Abdul Khali ‘Harmonize’ ameandika barua ya kutaka kutoka WCB, mkali wa Muziki na Filamu Bongo, amemfungukia msanii huyo kuwa ni mapema sana kujitoa.Akichonga na Showbiz, Sabby ambaye amejikita nchini Kenya akifanya shughuli zake za muziki alisema, alichokifanya Harmonize ameharakisha kwani bado hajajipanga vizuri.

“Kwa mtazamo wangu mimi naona Harmonize kuondoka WCB atafifia kama alivyovififia Mavoko.‼ Waliomshauri aondoke hawana lengo zuri na kama maslahi ndiyo shida hilo linazungumzika, mikataba irekebishwe alipwe zaidi, kuondoka WCB atakosa mvuto,” alisema Sabby