Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana amezitaka Taasisi na watu binafsi wanaomiliki silaha, kuzitunza sehemu sahihi ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kutokea endapo zitachukuliwa ama kuibiwa na kutumika vibaya.

Ameyasema hayo mara baada ya kijana mwenye umri wa miaka 19 Faisal Ibrahim, Mkazi wa Soko Kuu la Arusha, kujiua kwa kujipiga risasi kichwani katika paji lake la uso kwa kutumia bunduki aina ya Rifle Wichester inayomilikiwa na baba yake.

Aidha, kijana huyo mwenye asili ya Kihindi alijipiga risasi hiyo majira ya saa 05:00 alfajiri ya Agosti 18, huku chanzo cha tukio hilo kikielezwa kuwa ni msongo wa mawazo uliotokana na matumizi ya madawa ya kulevya.

Mwili wa kijana huyo umehifadhiwa katika hospitali ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi