Msanii nyota kutoka kundi la Wasafi Classic Baby (WCB), Raymond Shaban Mwakyusa ‘Rayvanny’ amesema anaamini kuwa Diamond pamoja na viongozi wa lebo ya Wasafi wanawapenda sana wasanii wao, vivyo hivyo wasanii wanapenda viongozi wao pia, hivyo kama kuna mikwaruzano na kupishana ni vyema ikamalizwa.

Amesema siku ikitokea wamesambaratika watakosa nguvu na hatimaye hawawezi kufika mbali kwa sababu umoja wao ndiyo nguvu yao.

Amewasihi mashabiki waendelee kuonesha upendo kwao ili wazidi kupata nguvu ya kufanya kazi nzuri zaidi na sio kusababisha chuki miongoni mwa wasanii wa kundi hilo.

“Wakimfuata labda Harmonize kwenye ukurasa wake, wakamtutukana na kumwambia umetoka Wasafi, sijui nini….! Maneno yanakuwa, anaweza akaona kwamba Wasafi wanamtukana au Wasafi wanatuma watu.”


Amesema wao ni kama familia na hakuna msanii yoyote anayetoka, msanii anayechukia viongozi na hata viongozi wanaochukia wasanii wao na kusisitiza kuwa angependa kuona wako vizuri na wanaendelea kuwa pamoja.

Amesema hata ikitokea msanii ametoka basi ndani ya moyo wake ataendelea kubaki na mapenzi na Wasafi na hata viongozi wakimfukuza msanii ndani ya kundi hilo basi wataendea kubaki na mapenzi naye.


Amesema umoja wao ndiyo nguvu yao na anaamini mashabiki wao wanawapenda sana na wataendelea kuwapa sapoti kwenye kazi zao.