Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, katika viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, ambapo jumla ya nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika SADC zinashiriki katika maonesho hayo kuelekea Mkutano Mkuu wa 39 wa Jumuiya hiyo unaotarajia kuanza Agosti 17 na kumalizika 18.

Mabanda ya maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, katika viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, ambapo jumla ya nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika SADC zinashiriki katika maonesho hayo kuelekea Mkutano Mkuu wa 39 wa Jumuiya hiyo unaotarajia kuanza Agosti 17 na kumalizika 18.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Kitengo cha Bandari Wakala wa Vipimo, Peter Chuwa (kulia) wakati alipotembelea banda la maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, katika viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko na Uhusiano Benki ya TIB Said Mkabakuli (wapili kushoto) wakati alipotembelea banda la maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, katika viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzanite Founder Foundation, Asha Ngoma (kushoto) wakati alipotembelea banda la maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, katika viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko na Uhusiano Benki ya TIB Said Mkabakuli (wapili kushoto) wakati alipotembelea banda la maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, katika viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Kitengo cha Bandari Wakala wa Vipimo, Peter Chuwa (kulia) wakati alipotembelea banda la maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, katika viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, akimsikiliza Ofisa Biashara na Masoko wa Kampuni ya Chai Kagera, Fredson Simon, wakati alipotembelea banda la maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, katika viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
---
Rais wa Zanzibar ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kufunga maonesho ya Viwanda vya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) leo Agosti 8, 2019.

Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dk.Hasani Abasi amesema baada ya maonesho hayo kufungwa wageni waliohudhuria watapata nafasi ya kutembelea maeneo ya viwanda ili kuangalia utekelezaji wake kwa vitendo.

“Katika ufungaji Dkt. Shein atafunga majira ya mchana na huku kesho kutwa baadhi ya wageni watapata fursa ya kutembelea viwanda kwa ajili ya kuangalia utekelezaji,”alisema.

Alitaja maeneo ambayo wageni hao watatembelea kuwa ni Unguja,Kibaha, Bagamoyo kwa ajili ya kuona Tanzania ilivyotekeleza kwa vitendo sera ya viwanda.

Pia Dkt. Abasi alitoa ratiba ya mkutano huo baada ya kufungwa leo kwamba kuanzia Agosti 9-12 kutakuwa na mkutano wa maofisa waandamizi wa nchi za SADC ambao ni makatibu wakuu.

Alisema katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,atakuwa Mwenyekiti na kujadili ajenda mbalimbali zilizopita.

Agosti 14, mwaka huu, kutakuwa na vikao vya mawazili wa nchi za SADC ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Profesa Palamagamba Kabudi atakuwa akichukua nafasi ya Uenyekiti wa baraza la Mawazili kwa nchi.

Agosti 15, mwaka huu kutakuwa na majadiliano ya ushirikiano wa kikanda ambapo Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa akauongoza na kuelezea uzoefu wake.

Dk. Abasi alisema majadiliano hayo yatafanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaammkwenye ukumbi wa maktaka mpya ya Taifa.

“Kiongozi huyo ataeleza uzoefu wake wa ushiriki kikanda na amekuwa akifahamu mambo mengi kuhusiana na SADC ambapo Agosti 16, mwaka huu kutaundwa muundo wa wa SADC wa masuala ya ulinzi na usalama,” alisema.

Alisema katika mkutano huo RaIS Dk. John Magufuli na Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete watahudhuria.

Vilevile alisema viongozi hao wataangalia changamoto za ulinzi na usalama kwa nchi za SADC na jinsi ya kuzisimamia.

Agosti 17 na 18 ndio utakapofanyika mkutano mkuu wa wqakuu wa nchi na serikali katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere na Rais Dk. Magufuli anatarajia kuongoza mkutano huo baada ya kuidhinishwa kuwa mwenyekiti wa SADC kiwa kipindi cha mwaka mmoja.

Kwa upande mwingine, Dk. Abasi alisema kupitia maonyesho ya Viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika alichojifunza ni kuona nchi za jumuiya hiyo zikifanya vizuri katika uzalishaji wa bidhaa za viwandani.

“Moja ya fursa ya kunufaika na SADC ni kwenda kujua bidhaa zinazozalishwa nchi za jumuiya hiyo aidha mtu azitumie kwa matumizi ya nyumbani au apate fursa ya nchi gani inahitaji bidhaa gani” alisema.