Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amepokea tausi wa nne (4) kutoka Tanzania.
Tausi hawa wanawasili Kenya kutokana na ahadi aliyopewa Kenyatta na Dkt John Pombe Magufuli, alipozuru Chato, Tanzania kwa ziara ya kibinafsi.



Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Pindi Hazara Chana na balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kazungu walikuwa katika ikulu ya Nairobi leo kumkabidhi tausi hao. “Hii ni ishara ya undugu na urafiki baina ya wakazi wa afrika mashariki. Inaleta heshima kubwa si tu kati ya Ma Rais bali kwa vizazi vya sasa na vijavyo” Uhuru Kenyatta Rais wa Kenya.