Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anatarajiwa kuwasili Nchini Jumatano ya August 14 kwa Mwaliko wa Ziara ya kitaifa (State Visit) ya siku mbili ambapo atapokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema Rais Ramaphosa atawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere majira ya Saa Tano usiku na baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili ataendelea kubaki Nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano Mkubwa wa Viongozi wa wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika SADC.

Aidha RC Makonda amesema Maraisi wa Mataifa mengine wataendelea kuingia Nchini kuanzia Agosti 16, ambapo amewataka wananchi kuwa wakarimu kwa wageni na kutumia vizuri fursa ya ujio wa Viongozi hao

kuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda