RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa na mkewe, Dkt. Tshepo Motsepe,  wamewasili nchini Tanzania usiku wa kuamkia leo na kupokelewa na mwenyeji wao, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabundi ambaye alimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli..


…Akilakiwa na Prof. Kabudi.

Ramaphosa amewasili kwa ziara rasmi ya siku mbili nchini kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ambao utaanza keshokutwa Jumamosi, Agosti 17, 2019 jijini Dar es Salaam.


…Akiongozana na  Prof. Kabudi.

 


…Akisalimiana na Mkuu wa Wilaya (DC) wa Ubungo, Kisare Makori.  Wengine kutoka kushoto ni DC wa Kinondoni, Daniel Chongolo; DC wa Kigamboni, Sarah Msafiri na DC wa Ilala, Sophia Mjema.




….Akisalimiana na DC Mjema.




…Akisalimiana na RPC wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa.