Rais Dkt John Pombe Magufuli ameitisha mkutano na Maafisa Watendaji wa Kata Tanzania Bara, unaotarajiwa kufanyika Ikulu, Dar es Salaam Septemba 2, 2019. TAMISEMI imewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa kuwaruhusu watendaji hao na kuwalipa posho za kujikimu na nauli ili wafike mkutanoni.