Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameipongeza Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kazi nzuri ya kuchunguza sampuli mbalimbali, kusimamia sheria za usimamizi wa kemikali na kudhibiti vinasaba vya binadamu.
Rais Magufuli ametoa pongezi hizo leo alipotembelea Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyopo Kivukoni Jijini DSM ambapo ameona jinsi mitambo ya uchunguzi vya kisasa inavyofanya kazi ikiwemo uchunguzi wa vinasaba vya miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya moto iliyotokea Mjini Morogoro tarehe 10 Agosti, 2019 baada ya lori lililobeba mafuta kupinduka na kisha kulipuka moto.