Jeshi la Polisi limevamia makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo yaliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam na kuzuia mkutano wa Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, aliokuwa aufanye leo Ijumaa, Agosti 16, 2019 na wanahabari ofisini hapo.
Polisi pia, wamemkamata Katibu wa Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu,  na kuelekea naye kituo cha Polisi Oyster Bay, jijini Dar es Salaam kwa mahojiano.

Naibu Katibu wa Uenezi ACT Wazalendo, Seif H. Suleiman,  amethibitisha tukio hilo na kusema magari mawili ya askari polisi wakiwa na silaha walifika ofisini hapo na kuzuia mkutano huo ambapo dakika takribani 15, waliondoka na Ado Shaibu.
Leo, Zitto Kabwe alitarajia kuongea na waandishi wa habari kuhusu Mkutano Mkuu wa 39 wa Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusdini mwa Afrika (SADC).
Mkutano huo umeahirishwa mpaka taarifa nyingine zitakapotolewa.