Picha adimu za mkewe mfalme wa Thailand aliyepewa wadhifa hivi karibuni zimetolewa na kasri, na inaarifiwa kusambazwa pakubwa mitandaoni.

Sineenat Wongvajirapakdi, mwenye umri wa miaka 34, anaonekana akiendesha ndege ya kivita , akiwa amevalia magwanda ya vita na kufyetua bunduki.

Wadhifa wa 'consort' aliopewa Sineenat hutolewa na mfalme kwa mkewe au na Malkia kwa mumewe.


Mfalme Maha Vajiralongkorn, mwenye umri wa miaka 67, alimpa heshima hiyo Sineenat mnamo Julai, miezi miwili baada ya kumuoa Malkia Queen Suthida, mkewe wa tatu.

Sineenat ni mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo katika karibu karne nzima, shirika la habari la AFP linaripoti.


Mtandao uliokuwa na picha hizo ulikabiliwa na matatizo baadaya watu wengi kujaribu kuingia kuzitazama pica hizo kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Wasifu wake umechapishwa karibu napicha hizo zake.


Katika taarifa yake, Kasri la Thailand linasema mfalme "aliagiza kuundwa kwa maelezo ya maisha ya kifalme" ya Sineenat, ambaye ni rubani wa kusomea, mhudumu wa afya na mlinzi binafsi.

Malkia Suthida - aliye na miaka 41- ni mhudumu wa zamani wa ndege na naibu mkuu wa kitengo cha ulinzi wa mfalme - ni mpenzi wa muda mrefu wa Mfalme Vajiralongkorn na ameonekana hadharani naye kwa miaka mingi.

Alitawazwa kuwa mfalme baada ya babake kufariki mnamo 2016.