Klabu ya Ittihad kutoka katika jiji la Alexandria nchini Misri imefanikiwa kukata mzizi wa fitna baada ya kumsainisha nyota Emmanuel Okwi wa Uganda.

Okwi aliyekuwa akiaminika atarejea Simba baada ya kushindwa kumalizana na klabu ya nchini UAE, ametua nchini Misri na kusaini mkataba wa had mwaka 2021.

Rais wa Ettihad Mohamed Mosselhi amesema Okwi wamemalizana naye na atacheza katika timu yake hadi mwaka 2021.


Hii ni timu ya pili ya Afrika Kaskazini, Okwi anasaini kuitumikia. Kabla aliwahi kuuzwa na Simba kwa Etoile du Sahel ya Tunisia na baadaye akarejea Simba kabla ya kuuzwa tena SønderjyskE Fodbold ya nchini Denmark.

Katika michuano ya Afcon iliyomalizika nchini humo, Okwi alikuwa ndiye mchezaji nyota zaidi katika kikosi cha timu ya taiga ya Uganda kilichofika hatua ya 16 Bora.