MGANGA hajigangi! Licha ya kwamba kwa sasa ameishika dini vilivyo, msanii wa filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nuru’ amewaomba watu wamuombee ili aweze kufika peponi.  Akibonga na Ijumaa,Nora alisema anaweza kuwa mstari wa mbele kuwahamasisha watu waache dhambi na kuyafuata anayopenda Mungu lakini asifike peponi kama watu wanavyotarajia.

“Unajua japo mimi natumia muda mwingi sana kwenye kurasa zangu za kijamii kuwahamasisha watu waache mabaya lakini wanaweza kuingia peponi wasinione hivyo nawaomba sana waniombee na mimi niweze kuuona ufalme wa Mungu nawaomba sana,” alisema Nora.