Staa wa muziki wa HipHop rapa Nikki Wa Pili amefunguka 'issue' za mastaa kupenda kudanganya umri na kuwavimbia mashabiki katika mitandao ya kijamii.


Nikki Wa Pili amefuguka hayo baada ya kumalizika kwa mkutano uliokutanisha wasanii wote, wanahabari chini ya waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Mh. Harrison Mwakyembe.

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, amesema, "Sababu ni nyingi hata kibiashara pia, Mtu anaweza kukujaji kutokana na umri wako kwa hiyo ina busara zake".

Aidha Nikki Wa Pili ameeleza kuhusu kauli aliyosema ni bora mastaa wawe wanajibu maoni 'comments' za mastaa wenzao kwenye mitandao ya kijamii kuliko kujibu watu wa kawaida.

"Nilikuwa namaanisha watu ambao hawana staha, mimi ni mmoja wa wasanii wanaowasiliana na watu wengi ila watu hao wanakuwa hawana staha, kama unapenda uwasiliane na mtu lazima uwe na ustaarabu, kama hakuna ustaarabu mahusiano yatavunjika na nafikiri nimewaambia ukweli sijawavimbia" amesema Nikki Wa Pili.