Wasalaam
Msanii wa muziki wa kufoka foka bwana Niki Mbishi akihojiwa na moja ya chombo cha habari aliulizwa mbona mwaka huu hajapata show yeyote ile hata kwenye tamasha la wasafi kama mwaka jana ? Msanii Niki mbishi alihamaki na kusema hajui kwanini yeye hajapewa show lakini aliendelea mbele na kusema waandaji wa Tamasha la wasafi wanatakiwa kujipanga kwani tamasha halina amsha amsha na wala halina mvuto kama mwaka jana walipokuwa kwenye tour..

Lakini mtangazaji alimuuliza mbona muamko unaonekana na watu wanajaa kila show na wadhamini wana miminika kuliko tamasha lolote maana hadi sasa lina wadhamini zaidi ya sita ....Nikki mbishi alijibu kwa kusema lakini ukweli ni kwamba tamasha halina mvuto na amsha amsha kama kipindi cha mwaka jana.....

Ni kweli Nikki mbishi anasema kweli?

By Ruttashobolwa/JF