Na Khadija seif, Michuzi tv
MSANII wakike wa Bongofleva anaefanya vizuri kimataifa Nandy (African princess) amesema hatosita kusaidia na kuwafikisha mbali wasanii chipukizi wa kundi la THT.

Nandy ameeleza kuwa moja ya ndoto za wasanii wengi wa Muziki nikuona wanashikwa mkono na kufika mbali kwani hata yeye anatambua mchango wa watu mbalimbali waliomuwezesha kufika alipo akiwataja Kama Msanii Dullysykse pamoja na Marehem Ruge Mutahaba.

"Wapo wasanii wengi ambao wanafanya vizuri kama Barnaba, linah, jaymelody, Benson, Amin pamoja na wengine wengi hao wato ni zao la tht waliweza kushikwa mkono hivyo nitajitahidi na Mimi niweze kuwashika mkono waliobakia,"

Aidha, Nandy amesema bado anaamini wakipewa fursa watafanya vizuri hivyo wakae tayari na waendelee kuvipigani vipaji vyao wasikate tamaa.

Hata hivyo amefafanua mafanikio aliyoyapata kwenye Tamasha lake la (Nandi festival ) kuwa limeweza kumjenga kiakili, kumkuza kisanii,limempa moyo sana na kumpa nafasi yakujua mashabiki wengi hasa mikoani.

"Imenipa nafasi kubwa sana ya kugundua kuwa wasanii wakike wanaweza kutoa burudani kisawasawa kutokana na kuwa na mashabiki wengi pamoja na hamasa katika kutoa burudani na ndio maana niliwakutanisha wasanii kama mwansiti, Rosa ree, Linah na Haitham pamoja na wengine,"

Hata hivyo ameweka wazi kuwa yeye na Msanii Dogo janja pamoja na Whozu ni rafiki zangu ambao  nashirikiana na kwenye vitu vingi hasa vya Muziki.