






Na Dixon Busagaga,Moshi
Spika wa Bunge, Job Ndugai, ametaja mambo 15 aliyofanya Rais John Magufuli kwa kipindi cha miaka minne alichokaa madarakani na kuwataka watanzania kumuunga Mkono.
Ndugai ameyataja mjini Moshi, wakati wa kongamano la kumpongeza Rais lililoandaliwa na Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT).
Hotuba ya Ndugai ilisomwa kwa niaba yake na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson , katika uwanja wa Majengo na kuhudhuriwa na wanachama wa UWT na wanawake wa mkoa huo.
Ndugai alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020, imetekelezwa kwa kiwango kikubwa,na kwamba miongoni mwa mambo ambayo ametekeleza Rais ni kurejesha nidhamu kwa watumishi.
Alisema lingine ni kushughulikia tatizo sugu la Rushwa ndani ya serikali,na ndani ya chama cha mapinduzi hali ambayo itapunguza kwa kiasi kikubwa rushwa ya uchaguzi katika Chaguzi zijazo.
Akizungumza mwenyekiti wa UWT Taifa, Gaudensia Kabaka, alisema kongamano hilo lililenga kumpongeza Rais kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha miaka minne na kwamba mambo makubwa yamefanyika katika kipindi hicho.