Moja ya vivutio katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro ni pamoja uwepo wa maji baridi katika maeneo ya Mlima yanayotokana na maporomoko.

Naibu Spika Dkt Tulia Ackson anayeendelea na safari ya kuelekea Kilele cha Uhuru akajaribu radha ya maji haya ambayo ndio chanzo cha maji katika mkoa wa Kilimanjaro likiwemo Bwawa la Nyumba ya Mungu.


Dkt Tulia na watu wengine 11 wanapanda Mlima Kilimanjaro ikiwa ni siku ya nne leo kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua Mashine za kutengeza Taulo za watoto wa kike yaani PADS kupitia taasisi ya Tulia Trust.