Mwasiti: Nandy Ana Akili, Atafika Mbali
MWANADADA mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, Mwasiti Almasi ‘Mwasiti’ ameibuka na kumsifia mrembo anayetikisa kwa sasa kunako Muziki wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ kuwa ni msichana mdogo lakini anajielewa hivyo akiendelea kuwa hivi basi atafika mbali kimuziki

Mwasiti aliendelea kusema kuwa tangu ameanza muziki hajawahi kuona msanii wa kike akijitoa kuandaa shoo kubwa kama alivyofanya Nandy ambaye hana muda mrefu kwenye gemu lakini ameweza kufanya mambo makubwa na yanayoonekana kwenye jamii.

“Nandy ni msichana mdogo sana lakini amethubutu kufanya vitu flani kwenye gemu na ameweza, hii ni tafsiri nzuri kwa wasanii wa kike Bongo kuwa tunaweza kama tukiwezeshwa.

“Niamini mimi huyu mtoto atakuja kufika mbali sana kimuziki kama ataendelea kuwa na nidhamu na upendo kwa mashabiki na wasanii wenzake, kama leo hii ameweza kuandaa Nandy Festival nakuchukua wasanii wenzake kibao tena wote wa kike huoni kama ni mwanzo mzuri?

Halafu ona hata anavyojaza shoo zake anatupa moyo hata sisi kwakweli,” alisema Mwasiti.