Mwanaume Afia Kifuani Mwa Mwanamke Wakishiriki Tendo la Ndoa kwenye Shamba la Mahindi
Mwanaume mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Julius Bor  (35) amefariki dunia akiwa katika shamba la mahindi katika Jimbo la Kapseret lililopo Kaunti ya Uasin Gishu nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Polisi Mjini Kapseret, Imeeleza kuwa kabla ya umauti, Julius Bor alikuwa na mama mmoja aliyejitambulisha kwa majina Misik Cheruto (40) wakinywa pombe za kienyeji na baadae walikubaliana kutoka kimapenzi.

Polisi wamesema baada ya makubaliano hayo,  Wawili hao waliingia katika shamba la mahindi ambalo lipo karibu na nyumba waliyokuwa wanakunywa  na kufanya mapenzi.

Mwanamama Misik Cheruto ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi, Amesema kuwa Mwanaume huyo alianguka kifuani mwake baada ya tendo la  ndoa .