Mwanamitindo na staa wa ubunifu wa mavazi na mfanyabiashara nchini Nigeria Toyin Lawani (37), ametangaza kutaka kuoelewa na Wanaume watatu atakapofikisha miaka 40.

Toyin Lawani ametangaza hivyo kupitia Insta Stori ya mtandao wa kijamii wa Instagram, kuwa yupo tayari kuwajengea nyumba na kuishi nao wote wa watatu kwa pamoja.

Toyin Lawani ameandika kuwa "Kwanini Wanaume wanaruhusiwa kuoa Wanawake watatu na zaidi, mimi nitakapofikisha miaka 40, nitaolewa na wanaume watatu tofauti kwa pesa zangu mwenyewe, nitajenga nyumba kubwa na kuishi nao ila nitakuwa nachagua kila Mwanaume mmoja wa kulala naye kwa kila usiku mmoja".

Pia ameendelea kuandika, ''wanaume wanaaminishwa kuoa wanawake wengi, kwanini wanawake washindwe na sasa hivi dunia imebadilika na wanawake wanatakiwa waheshimiwe''.

Mwisho kabisa ameandika kuwa Wanawake hawawezi kupata ujauzito bila Wanaume, ila wana uwezo wa kununua mbegu za uzazi, mwanamke anabeba mimba kwa miezi 9, miaka miwili ya kumlea mtoto, Mwanaume hawezi kumpa mtoto zawadi wala hajali ila  anaweza kukusaliti.