Mwanaheri Silitumii Vibaya Shepu Langu
WANADADA anayekimbiza kwenye Tamthiliya ya Kapuni, Mwanaheri Ahmed amefunguka kwamba anajijua kuwa ameumbika lakini kamwe hawezi kujilengesha kwa wanaume wakware.  Akipiga stori na Gazeti la Amani, Mwanaheri alisema mara nyingi akikaa kwenye kioo huwa anajiangalia na kuishia kumshukuru Mungu kwa uumbaji wake lakini kamwe hawezi kujirahisi  licha na kutamaniwa na wanaume wengi.

“Ninajijua kuwa nina lishepu zuri, tena mara nyingi nikiwa najiangalia kwenye kioo najizungusha nyuma na mbele, kisha naishia kusema asante Mungu kwa uumbaji wako, ameniumba haswa na mimi ni mzuri bwana ndio maana niliwekwa ndani,” alisema Mwanaheri ambaye aliolewa mapema mwaka jana na mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina moja la Hamisi