BLUE Ivy ambaye ni mtoto wa mastaa wanaokimbiza kwenye Muziki wa R&B na Hip Hop kutoka Marekani, Jay-Z na Beyonce, amefuata nyayo zao  kwa kuvunja rekodi kwenye ‘chart’ za Billboard.  Blue Ivy amevunja rekodi ya kuwa mdogo zaidi kuwahi kuingia katika chart za Billboard Hot 100 akiwa na miaka 7 tu jambo ambalo halijawahi kufikiwa na mtoto yeyote.

Mtoto huyo ameingia katika chart hizo kupitia ngoma alioshirikishwa na mama yake, Brown Skin Girl ambayo pia wapo SAINt JHN na Wizkid. Ngoma hiyo kwa wiki hii imeshika namba 76 na inatabiriwa kuzidi kupanda zaidi ya hapo. Ikumbukwe kuwa wazazi wake wote wawili walishawahi kuingia kwenye chart hizo mara kibao