Polisi wa Jiji la Logos nchini Nigeria, wamemkamata msanii na mtayarishaji wa muziki nchini humo Tekno Miles pamoja na wasichana wawili.
Polisi wamesema wamemkamata staa huyo kwa sababu ya kumuuliza maswali na kumfanyia uchunguzi kwa tukio ambalo amelifanya wikiendi iliyopita.
Wikiendi iliyopita zilienea video katika mitandao ya kijamii zikionyesha Tekno akiwarekodi wasichana watatu wakiwa wanacheza huku nusu ya maungo ya miili yao yakiwa wazi na yeye akiwatunza pesa.
Siku ya Jumapili Tekno aliomba msamaha kwa kutumia barua baada ya kufanya tukio hilo na amesema wasichana hao amewatumia katika video yake mpya itakayotoka siku za hivi karibuni, na wala hakuwa na nia mbaya kuwarekodi video hizo.