Baada ya watu kusema sana anameza vidonge ili awe mweupe! Hatimaye video vixen, Irene Louis ‘Lyyn’ ameanika ukweli wa madai hayo kuwa muonekano wake wa ngozi ndivyo alivyo tangu amezaliwa.Lyyn aliyajibu hayo alipobananishwa kati na Mikito Nusunusu pande za Mlimani City jijini Dar ambapo alisema amekuwa akisikia na kuona mitandaoni akiandamwa na maneno ya watu ambao hawajui ukweli kwani kwao wengi ni weupe kama alivyo.

“Unajua nachoka na haya maneno ya watu, yaani kila siku ni mimi tu, kwa nini jamani? Ukweli ni kwamba nilivyo sijawahi kutumia hayo madawa. Halafu vitu vingine rahisi sana kama wanaamini natumia nimekuwa hivi basi na wao waingie madukani wanunue wawe kama mimi,” alisema Lyyn.