ULE usemi usemao abiria chunga mzigo wako, umejidhihirisha wazi kwa msanii mkongwe Yvonne Cherry ‘Monalisa’ baada ya kumtaha-dharisha muimbaji wa Injili, Emmanuel Mbasha kwa mtoto wake, Sonia.  Ishu ilianza hivi; Mona alitupia picha ya mtoto wake kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram akikata keki kwa niaba yake mara akatokea Mbasha na kutupia komenti ‘ankooo huyo’ akarudishiwa jibu na Mona ‘hiyo anko vipi baba’.

Akizungumza na Ijumaa, Mona alieleza sababu za kumjibu Mbasha hivyo ni kwa sababu siku hizi ukiachia anko nyingi kwa watoto baadaye kuna madhara. “Nilimtahadharisha Mbasha mapema na kumwambia hizo anko ziishie kwenye instagram na ujumbe kaupata maana siku hizi mtu akimuita mwanao anko muangalie mara mbilimbili anaweza kumsababishia madhara baadaye,” alisema Monalisa.