Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara ameghairisha mkutano wake na waandishi wa habari ambao alipanga kuufanya hii leo katika ukumbi wa Serena Hotel.

Kupitia akaunti yake ya Instagram hapo jana, Manara alitangaza kufanya mkutano na waandishi wa habari katika hotel ya Serena jijini Dar Es Salaam lakini ghafla asubuhi ya leo ameughairisha huku akitoa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wake.

”Sorry kwa Wanahabari, Press iliyokuwa ifanyike leo Serena Hotel imehairishwa baada ya dharura iliyotokea ambayo ipo nje ya uwezo wetu, Tutawaarifu kitakachojiri  Haji Manara 🙏.” Ameandika Haji Manara.

Ujumbe wa Haji Manara hapo jana akiwatangazia wanahabari kuwa kesho (leo) angefanya mkutano nao ambao angezungumza mambo mbalimbali.

”Kesho Jumanne tarehe 27/8/2019 Saa sita kamili mchana,Kwenye hoteli ya nyota tano ya Serena iliyopo hapa jijini Dar es Salaam,nitaongea na Wanahabari za michezo,” Ameandika Haji Manara.

Haji Sande Manara ameongeza ”Mkutano huo utafanyika Kwenye ukumbi wa kivukoni three uliopo ndani ya hoteli hiyo Mkutano huo utarushwa live na @azamtvtz kupitia Azam sports two na pia Kwenye Page zangu za Social Media
Karibuni.”

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na sito fahamu hasa kuhusu nafasi ya Afisa habari wa Simba SC ambayo ipo chini ya Haji Manara akidaiwa tayari imeshapatiwa mtu mwingine ambaye atakuja kutangazwa hivi punde.

Hata hivyo hii ni mara ya pili sasa kwa siku za hivi karibuni kwa, Haji Manara kupanga kufanya mkutano na wanahabari kisha kushindikana inaonekana kuwa hata mkutano wake wa leo alifahamu wazi hautafanikiwa kufanyika.

Macho na maskio ya wapenzi wa soka na mashabiki wa Simba wanasuburi kusikia lolote kutoka kwa uongozi hasa kuhusu nafasi hiyo ya Afisa Habari pamoja na matokeo waliyopata katika mchezo wa klabu bingwa barani Afrika baada ya kutolewa kwa aibu kubwa na UD Songo hasa ukilinganisha na usajili wa Simba, upana wa kikosi, uwezo wao na malengo waliyojiwekea msimu huu ambayo ilikuwa ni kufika hatua ya nusu fainali baada ya msimu uliyopita kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.