Ikiwa tayari mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2019 yamekamilika na mshindi kutangazwa ambaye ni Sylivia Sebastian Bebwa sasa leo August 27, 2019 Miss huyo amekaa kwenye mahojiano na Clouds FM kwenye kipindi cha leo tena na kuzungumzia utayari wake wa kupambana kwenye Miss World.

Hata hivyo Basila Mwanukuzi ambaye ni mwaandaji wa mashindano hayo amezungumza kuhusu zawadi ya mwaka huu kuwa tofauti na miaka mingine na kusema kuwa zawadi ya pesa ni nzuri na kwa mwaka huu wameangalia kitu cha tofauti ukiangalia na miaka mingine iliyopita na ndipo wakafikia maamuzi ya kiasi cha pesa.

“Gari ni zawadi nzuri lakini pesa ni zawadi nzuri sana, tuliangalia kitu cha tofauti kwa mwaka huu, na chanzo cha magari ilikuwa ni Mdhamini maana zamani ili mdhamini aonekane ametoa zawadi hivyo walikuwa wanatoa gari. Mwaka huu hatukuwa na mdhamini hivyo nikaona sio vibaya kutoa pesa ili iweze kumsaidia yeye kwenye baadhi ya ndoto zake” >>>Basila Mwanukuzi“Changamoto kubwa kwangu kwanza ilianza kwa Mama yangu maana alikuwa muoga sana na alikuwa anaona kama ananitelekeza kwenye dunia, kingine kambini maana nilikutana na warembo wengi na kati ya warembo 20 mmoja ndiyo anatakiwa kuchukua taji la Miss Tanzania, hilo ndiyo ilikuwa changamoto kubwa maana ukiangalia wote wazuri na wanaakili hivyo kuna muda unawaza kweli nitashinda”

“Naamini nikienda Miss World nitafanya vizuri, kikubwa ambacho nakitaka kutoka kwa wananchi ni support yao, maana kama nikiwa na support ya kutosha taji lazima lirudi nyumbani, upande wangu nimejipanga vizuri na tayari nishaanza kujipanga na project mbalimbali za Miss World” >>>Sylvia Sebastian Miss Tz 2019