Aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 2018/2019, Queen Elizabeth Makune amefunguka tofauti aliyokuwa nayo kabla ya kuwa Miss Tanzania na ishu ya kubadilisha gari.


Queen Elizabeth Makune amesema hayo akiongea na EATV & EA Radio Digital katika mashindano ya kumtafuta Miss mpya wa Tanzania 2019/2020 ambapo amesema.

“Kabla ya kuwa Miss Tanzania nilikuwa msichana wa kawaida tu, ila sasa hivi nasimama na kutizamwa na watu wengi, na kuhusu lile gari kutobadilisha au nembo ni sehemu ya Miss Tanzania kwamba nikipita mjue nimepata na nitaacha hivyohivyo sitabadilisha wala kutoa zile nembo”.

Aidha Queen Elizbeth Makune amesema tutegemee kumuona katika tasnia ya muziki na uigizaji kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu na Aunty Ezekiel.

Pia ameendelea kusema kuwa kwa sasa tayari amekuwa staa, yupo kotekote na kama fursa anaiweza atafanya.