Kaka wa msanii Ice Boy aitwaye Elly Fire ambaye ni mbunifu wa mavazi hapa nchini Tanzania, amenyoosha maelezo kwa kumponda msanii Jux kuwa hajui kuvaa.Elly Fire amesema hayo kupitia Friday Night Live "FNL" ya EATV, baada ya kuulizwa kati G-nako warawara na Jux nani mkali wa kuvaa anayekwenda na mitindo zaidi.

"Mimi naona ni Gnako, Jux hajui kuvaa ila anafanya biashara, mimi napenda msanii anayevaa nguo ambayo inaishi, ukikutana na G nako au mimi utaona tuna muonekano wa kamera lakini Jux utakuta amevaa bidhaa zake".

Pia mbunifu huyo ameendelea kufunguka kuwa hakuna mtu ambaye angeweza kusema kama sio yeye, kwa sababu watu wengi walikuwa wanamkubali na wasanii wengi wanamuiga ambao walikuwa wanapotea ila amewarudisha kwenye ramani.

Mbunifu huyo wa mwanamitindo, tayari ameshafanya kazi za kuwavalisha wasanii kama Barnaba Classic, Country Boy, Mr T-Touch na Ice Boy.