Mbunge wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimajaro,Dk.Mathayo David Mathayo akimkabidhi Afisa elimu Kata, Ruth Kisaka Mifuko 250 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na mabweni katika kata ya Msimbo wilayani Same, ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 2020.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimajaro,Dk. Mathayo David Mathayo akimkabidhi fedha taslim Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mshewa, Anastazia Clement kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya kata hiyo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimajaro,Dk.Mathayo David Mathayo akimkabidhi fedha taslimu diwani wa CCM kata ya Mhezi wilayani Same John Kiure kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya kata hiyo.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimajaro,Dk.Mathayo David Mathayo akihutubia wananchi. 
MBUNGE wa Jimbo la Same Magharibi CCM, Dk. Mathayo David Mathayo amewaomba wananchi wa Jimbo la Same Magharibi kumuunga mkono na kumuombea afya njema Rais John Magufuli ili aweze kuendelea kuiongoza Tanzania izidi kupata maendeleo na kurudisha nidhamu katika sekta mbalimbali nchini.

Dk. Mathayo ametoa kauli hiyo katika siku ya kwanza ya ziara yake ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 kama alivyoahidi wakati akiomba ridhaa ya kuwaongoza wananchi wa jimbo hilo ambapo akizungumza na wananchi wa kata za Msindo, Mshewa na Mhezi, Mathayo amesema serikali ya awamu ya tano imeonesha mafanikio lukuki katika Nyanja mbalimbali.

Aidha Mbunge huyo amekabidhi vifaa mbalimbali alivyoahidi katika kata hizo zikiwemo Fedha, saruji na mabomba ya kusambazia maji huku akitoa rai kwa uongozi wa kila Kata kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika ndani ya kipindi cha miezi mitatu.

Katika Kata ya Msindo Dk. Mathayo ametoa fedha ,mifuko ya saruji,mabomba ya maji, ambapo katika kata ya Mshiwa amekabidhi mifuko ya saruji na fedha taslimu kwa ajili ya shughuli za marendeleo kiasi cha shilingi milioni 13 laki 9 na Zaidi ya shilingi million tisa katika kata ya Mhezi Zaidi ya shilingi milioni tisa na mifuko ya saruji.