Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika ibada ya kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali ya moto wa lori la mafuta lililoanguka katika eneo la Msamvu mjini Morogoro. Ibada hiyo ilifanyika kwenye viwanja vya hospitali ya mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole , Shukuru Fabian ambye ni mmoja wa majeruhi wa ajali ya moto wa lori la mafuta lililopinduka katika eneo la Msamvu mjini Morogoro. Aliwajulia hali majeruhi wa ajali hiyo kwenye hospitali ya mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimjulia hali, Hans Kifah ambaye ni mmoja wa majeruhi wa ajali ya moto wa lori la mafuta lililopinduka kwenye eneo la Msamvu mjini Morogoro. Aliwajulia hali majeruhi wa ajali hiyo kwenye hospitali ya mkoa wa Morogoro, Agosti 11, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NA K-VIS BLOG/Morogoro.

Awamu ya kwanza ya miili ya watu waliofariki dunia kwenye ajali ya mlipuko wa lori la kubeba mafuta imezikwa jioni hii Jumapili Agosti 11, 2019 baada ya vinasaba (DNA) kuoana kati ya waliofariki na ndugu zao.

Mazishi hayo yaliongozwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kwenye eneo la Kola Hill nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro ambapo awali aliwatembelea majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa kwenye hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro na kisha kushiriki ibada ya kuwaombea marehemu katika uwanja wa Shule ya Sekondari Morogoro.